• 1. Roho Mtakatifu Hufanya kazi kupitia ahadi ya Neno la Mungu (Matendo 1:4-8)
    Jan 13 2023

    Hapo mwanzo nilipatwa na tukio la kujiwa na miale ifananayo kama Roho Mtakatifu wakati wa maombi. Lakini miale hii haikudumu kwa muda, hivyo punde ilitoweka mbele ya kitita cha dhambi. Ingawa leo napenda kukuonyesha ukweli kuhusu Roho Mtakatifu ambaye atakaye kaa ndani yetu hata milele, si kwakupitia roho zidanganyazo ambazo hutambulika kwa dhambi, bali kupitia injili ya kweli. Roho Mtakatifu nitakaye mtambulisha kwako kwa kupitia ujumbe huu si kitu fulani unacho weza kupokea kwa maombi bali kupitia imani katika injili ya majina Roho tu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    16 mins
  • 2. Je, inawezekana mtu kumnunua Roho Mtakatifu kwa uwezo wake? (Matendo 8:14-24)
    Jan 13 2023

    Husika na somo kuu katika kifungu hiki, napenda kuleta ujumbe huu iwapo “mtu anaweza kumpokea Roho Mtakatifu ndani yake kwa kupitia juhudi binafsi”. Mitume katika nyakati hizo za Kanisa la kwanza waliweza kupokea nguvu toka kwa Mungu na kutumwa sehemu kadhaa naye. Yapo matendo ya miujiza kadhaa katika Kitabu cha Matendo, mojawapo likiwa kushuka kwa Roho Mtakatifu juu ya waumini pale Mitume walipowawekea mikono. Biblia inasema “Mitume walipowawekea mikono wale ambao hawakuwa wamempokea Roho Mtakatifu ingawa walikwisha mwamini Yesu, walipokea Roho Mtakatifu.”

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    57 mins
  • 3. Mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini? (Matendo 19:1-3)
    Jan 13 2023

    Aina gani ya Injili Paulo alihubiri? Alihubiri Injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake. Matendo 19:1-2 inasema “Ikiwa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akiisha kupita kati ya nchi za juu akafika Efeso, akakutana na Wanafunzi kadhaa wa kadha huko akawauliza, Je, mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Hata hivyo watu hawa walikuwa wamekwisha mwamini Yesu huku wakiwa wameweka kando maana ya ubatizo wa Yesu. Hawakujua juu ya Injili njema ambayo hupelekea kumpokea Roho Mtakatifu ndani. Na hii kupelekea Paulo kuuliza “Je, mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” lilikuwa swali geni kwa baadhi ya wafuasi. Watu wengine wangeliweza kuuliza “Je, una mwamini Yesu?” Lakini Paulo aliuliza swali katika njia isiyokuwa ya kawaida ili kwamba waweze kumpokea Roho Mtakatifu, ndani yao kwa kufanya upya imani zao katika Injili njema. Huduma ya Paulo ilikuwa ni kuhubiri Injili njema ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    19 mins
  • 4. Wale walio na imani sawa na Mitume (Matendo 3:19)
    Jan 13 2023

    Kwa kuangalia wafuasi wa Yesu Kristo kiwango cha imani zao walipokuwa na Roho Mtakatifu ndani yao ni tofauti kabisa na imani zao walipokuwa hawajawa na Roho huyo. Miili yao haikuonekana kuwa tofauti lakini baada ya kumpoke Roho Mtakatifu maisha yao yalibadilika kabisa kwa nuru ya Yesu Kristo.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    26 mins
  • 5. Je, unataka kuwa na Ushirika na Roho Mtakatifu? (1 Yohana 1:1-10)
    Jan 13 2023

    Ikiwa unahitaji kuwa na usharika na Roho Mtakatifu kwanza kabisa lazima uelewe kwamba dhambi iliyo ndogo kabisa mbele ya Mungu inatosha kutokufanya usharika na Mungu. Unaweza kudhani “Sasa itawezekanaje mtu asiwe na dhambi hata kidogo mbele ya Mungu?” Lakini ikiwa kweli unatamani usharika na Bwana basi lazima pasiwepo na kiza moyoni mwako. Hivyo ili uwe na usharika na Bwana, unahitajika kujua kwamba lazima uamini Injili ya ukombozi na kujitakasa dhambi zako zote.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    41 mins
  • 6. Amini ili Roho Mtakatifu akae ndani yako (Mathayo 25:1-12)
    Jan 13 2023

    Katika kifungu kilichopita hapo juu tumeona wanawali watano wenye busara na wapumbavu, wanawali wapumbavu waliwaomba wale wenyebusara kuwagawia kiasi cha mafuta ya taa lakini wenye busara wakawajibu wale wapumbavu “hayatatutosha sisi na ninyi shikeni njia muende kwa wauzao mkajinunulie”. Hivyo wakati wale walio wapumbavu wakienda nje kununua mafuta hayo, wale wenye busara walikuwa nayo katika taa zao na kuingia katika sherehe za harusi. Sasa basi ni kwa namna gani tunaweza kuyatayarisha mafuta kwa ajili ya Bwana? Kitu pekee tunachoweza kufanya ni kuusubiri msamaha wake wa dhambi katika mioyo yetu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    29 mins
  • 7. Injili iliyo njema inayowezesha Roho Mtakatifu kukaa ndani ya wanao amini (Isaya 9:6-7)
    Jan 13 2023

    Ili kumpokea Roho Mtakatifu tunahitajika kuwa na imani katika injili ya maji na Roho. Bwana wetu ameitwa wa Ajabu, Mshauri na Mungu mwenye Enzi. Bwana wetu amejitambulisha ndiye njia ya kwenda Mbinguni. Yesu Kristo amempatia kila mmoja zawadi ya Inijili njema.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    57 mins
  • 8. Kupitia nani maji ya uzima ya Roho Mtakatifu hutiririka? (Yohana 7:37-38)
    Jan 13 2023

    Maji ya uzima ya Roho Mtakatifu hutiririka toka mioyo ya wale wote wanao amini injili njema. Yohana 7:38 inasema “Aniaminiye mimi kama vile maandiko yalivyonena mito ya maji yaliyo hai itatiririka ndani yake.” Maana yake ni kwamba upo wokovu wa kweli na ondoleo la dhambi kwa wale wote wenye kuamini injili njema ambayo Mungu ametupatia.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    47 mins