• 1. Ni Lazima Uifahamu na Kuiamini Huduma ya Yohana Mbatizaji (Marko 1:1-2)
    Jan 24 2023

    Marko 1:2 inasema, “Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako.” Ndugu zangu waamini, unaweza kuipata haki ya Mungu ikiwa tu utatupilia mbali uelewa wa kale na kuifuata Biblia kadri Neno la Mungu linavyokuongoza. Hivyo, wakati unaposoma Neno la Mungu, ni lazima ulisome hali ukiwa umeyaacha mawazo na tamaa zako za mwili. Ni kwa kufanya hivyo tu ndipo unapoweza kutambua na kuamini katika mapenzi ya Mungu ambayo anataka kuyatimiza. Kanuni hiyo inatumika pia katika kifungu cha Maandiko cha leo. Ni pale tu utakapokuwa umeyaachilia mbali mawazo yako ya kimwili na kisha ukalifuata Neno la Mungu linapokuongoza ndipo unapoweza kufahamu kiusahihi huduma ya Yohana Mbatizaji na huduma ya Yesu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    35 mins
  • 2. Yohana Mbatizaji Hakushindwa (Mathayo 11:1-14)
    Jan 24 2023

    Ni huduma gani hasa ambayo Yohana Mbatizaji aliitimiza kabla ya Yesu? Wakristo wengi leo hii hawamfahamu vizuri Yohana Mbatizaji, hivyo wanatakiwa kupata mtazamo mpya kuhusu Yohana Mbatizaji ili waweze kumfahamu na kuikubali huduma yake kikamilifu. Sisi sote tunapaswa kuwa na ufahamu sahihi na kuukubali uhusiano kati ya huduma ya Yesu na ile ya Yohana Mbatizaji. Kwa kuufahamu uhusiano huu kikamilifu, basi unapaswa kwanza kulipokea ondoleo la dhambi kwa imani.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    1 hr and 5 mins
  • 3. Yohana Mbatizaji, Aliyekuja Katika Njia ya Haki (Mathayo 17:1-13)
    Jan 24 2023

    Kifungu cha Maandiko cha leo kinatoka katika injili ya Mathayo 17:1-13. Kifungu hiki kinaeleza kuwa Yesu aliwachukua wanafunzi watatu, Petro, Yakobo, na Yohana na akawaongoza kwenda katika mlima mrefu sana. Jambo la kushangaza lilitokea kule mlimani. Musa na Eliya walishuka toka Mbinguni. Na mavazi ya Yesu yalibadilika yakang’aa na kuwa meupe na sura yake ikabadilika pia. Yesu alizungumza na Musa na Eliya. Petro alipoona hivyo, akazungumza katika hali kindoto, “Na tufanye vibanda vitabu: kimoja chako, kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. Tunapenda kujenga vibanda vitatu na kuishi pamoja nawe.” Kisha wingu likawafunika na sauti ikasema, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye!”

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    47 mins
  • 4. Itazame Huduma ya Yohana Mbatizaji! (Luka 1:17-23)
    Jan 24 2023

    Injili ya Luka katika sura ya 1 aya ile ya 17 inaeleza kuwa Yohana Mbatizaji alikuwa ni mtu aliyekuja katika roho na nguvu ya Eliya na akaifanya kazi ya kuwarudisha watu kwa Mungu mbele ya uwepo wa Bwana. Yohana Mbatizaji alikuwa ni tofauti na watu wengine tangu alipozaliwa. Sisi watu wa kawaida tunaoana na kisha kuzaa watoto kwa kudhamiria au kutodhamiria kadri muda unavyozidi kwenda. Lakini Yohana Mbatizaji ni mtu ambaye kuzaliwa kwake kulikwisha tabiriwa na kuandaliwa katika Agano la Kale. Inasemwa kuwa Yohana Mbatizaji atakuja kwetu katika roho na nguvu ya Eliya.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    58 mins
  • 5. Tuufurahie Utukufu wa Mungu Kwa Shukrani (Yohan 1:1-14)
    Jan 23 2023

    Injili ya Yohana, Vitabu vitatu vya 1, 2, na 3 Yohana, na Kitabu cha Ufunuo ni Maandiko yaliyoandikwa na Mtume Yohana. Kwa kupitia Maandiko haya, basi tunaweza kuona jinsi imani ya Mtume Yohana ilivyokuwa, na pia jinsi imani ya wanafunzi wa Yesu ilivyokuwa. Mtume Yohana aliamini kuwa Yesu alikuwa ni Mungu halisi aliyeumba ulimwengu wote na sisi wanadamu, na kwamba Mungu alikuwa ni Mwokozi wake na Mwokozi wa wanadamu wote. Sisi sote tunapaswa kuwa na aina hii ya imani.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    56 mins
  • 6. Je, Unazifahamu Huduma za Watumishi Wawili wa Mungu? (Yohana 1:30-36)
    Jan 23 2023

    Kifungu cha maandiko cha leo kinatoka katika injili ya Yohana 1:30-36. Watumishi wa Mungu wanaoamini katika injili ya maji na Roho wanafahamu wote kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu na Mwokozi wa wenye dhambi. Vivyo hivyo, wale ambao wanamfahamu na kumwamini Mungu kwa kweli wanaweza kutambua kuwa Yohana Mbatizaji aliitimiza huduma muhimu na ya thamani akiwa kama mtumishi wa Mungu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    52 mins
  • 7. Kwa Nini Yesu Alipaswa Kuupokea Ubatizo? (Yohana 3:22-36)
    Jan 23 2023

    Watu wengi hawafahamu ni kwa nini Yesu alikuja hapa ulimwenguni na akaupokea ubatizo toka kwa Yohana Mbatizaji. Lakini ni lazima tufahamu vizuri kuhusu dhumuni la ubatizo ambao Yesu aliupokea, kuhusu Yohana Mbatizaji ambaye alimbatiza Yesu, na kuhusu uhusiano kati ya watu hao wawili. Kwa hiyo, kwanza kwa kutumia aya za Maandiko ninataka kuangalia habari za msingi na dhumuni la ubatizo wa Yesu uliotolewa na Yohana Mbatizaji katika Mto Yordani. Na ili kufanya hivyo ni lazima tugeukie katika Injili ya Mathayo na kisha kumchunguza Yohana Mbatizaji aliyembatiza Yesu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    1 hr and 1 min
  • 8. Ieneze Injili ya Kweli na Tendo la Haki la Yesu (Mathayo 3:1-17)
    Jan 23 2023

    Ni hakika kuwa Yohana Mbatizaji alikuwa ni mtu muhimu sana katika Biblia. Yohana Mbatizaji aliwalilia watu wa Israeli ili wafanye toba. Ni lazima tuzikumbuke kikamilifu kazi za Yesu na Yohana Mbatizaji. Yesu, aliyekuja hapa duniani aliwaokoa wanadamu, akitii mapenzi ya Mungu wakiwa pamoja na Yohana Mbatizaji. Yohana Mbatizaji na Yesu walikuja hapa duniani na wakayakamilisha matendo ya haki.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show more Show less
    24 mins